logo

PORALG

Students

FR
Fred Kibanofred.kibano@tamisemi.go.tz
0
0
0
Comments
0

MHE. CHATANDA  AMPONGEZA RAIS KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI RUFIJI

Na Mwandishi Wetu..

Mwenyekiti wa UWT- CCM Taifa, Mhe. Mary Pius  Chatanda amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 25 inayotekelezwa  wilayani Rufiji na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha  kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Mbali  na kumpongeza Mhe. Rais Samia, pia amempongeza Mbunge wa Rufiji kwa kusimamia utekelezaji wake ambapo amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na ina tija kubwa kwa wananchi.

"Hapa naomba niungane na watanzania wote kumpongeza Rais wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ambayo ameifanya nchi nzima, na hapa leo Rufiji tunashuhudia  kazi nzuri ambayo imetekelezwa kupitia miradi hii" amesisitiza Mhe Chatanda

Mhe Chatanda ambaye yupo kwenye ziara ya siku mbili katika  jimbo la Rufiji amekagua  mradi wa ujenzi wa daraja la Mbambe linalojengwa kwa urefu wa mita 81 na ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha  barabara kuu ya kilomita 3 itakayogharimu  bilioni 24.1.

Mkataba wa daraja hilo  ulisainiwa na  Wakala wa Barabara Tanzania na Mkandarasi M/S  Nyanza  Road Works Ltd  ya Mwanza ambapo kazi hiyo inatarajia kukamilika katika kipindi Cha miezi 6 kuanzia sasa.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa daraja hilo Mhe. Mchengerwa alifafanua  kuwa mradi wa ujenzi wa daraja hilo ni moja ya mikakati ya Serikali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii wilayani Rufiji maeneo jirani.

Rashid Salum Mkazi wa Ikwiriri amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo ambapo amesema kukamilika kwake kutakuwa msaada mkubwa kutokana na adha kubwa walihokuwa wakipata hapo awali.

Aidha, Mhe. Chatanda ameshuhudia utiaji saini wab mikataba ya ujenzi wa miradi ya maji  katika vijiji vya Mloka, Mbinju Mvuleni na Ndundutawa ambapo pia ameshuhudia zoezi la kupewa mabati 45 na Mhe. Mbunge  vijana wa bodaboda wa kijiji cha Mloka ili kuezekea eneo la kuegesha bodaboda zao.

Akitoa taarifa ya mradi huo, Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( RUWASA) Wilaya ya Rufiji Mhandisi Alkam Omari pamoja na uwekezaji mkubwa ambao  umefanywa na Serikali katika  kuwapatia wananchi maji safi na salama, mahitaji ya maji yamezidi kuongezeka ambapo amesema mradi huu unakwenda kuwa suluhisho.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu
Habari na Matukio