logo

PORALG

Students

AN
Angela Msimbilaangela.msimbila@tamisemi.go.tz
0
0
0
Comments
0

Miradi yote ngazi ya msingi itangazwe kupitia nest

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wakurugenzi  wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na wakuu wa vitengo vya manunuzi kuhakikisha miradi yote inayotekelezwa kwenye ngazi ya msingi inatangazwa kupitia mfumo wa Nest.

Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati akizungumza na Wabunge,Wakurugenzi wa Halmashauri, Makatibu Tawala Wasaidizi Miundombinu na wakuu wa vitengo vya manunuzi kutoka kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa kikao kazi kuhusu mfumo wa Nest kilichofanyika kwenye ukumbi wa wa Mabeyo jijini Dodoma leo tarehe 04.02.2024.

Amesema baada  kupata mafunzo haya  leo hii nendeni mkabadilike, fuateni Sheria ya Manunuzi, onyesheni mabadiliko hayo kwenye utekelezaji wa miradi na kuanzia sasa miradi yote itangazwe kupitia mfumo wa Nest na si vinginevyo alisisitiza.

Miradi hiyo ikishatangazwa kupitia Nest hakikisheni mnaisimamia kwa Weledi wa hali ya juu na kwa uaminifu ili itekelezwe kwa viwango vinavyotakiwa na thamani ya fedha iweze kuonekana’ amesema! 

Aidha Mhe. Mchengerwa aliwataka  PPRA kuhakikisha inawajengewa uwezo watumiaji wa mfumo wa Nest katika ngazi za msingi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati wa kuomba zabuni mbalimbali.

Comments

Please sign in to leave a comment.

Matangazo Muhimu
Habari na Matukio